Mfahamu Jongoo

Kiumbe mdogo aliyejipatia umaarufu kwa kuwa na miguu mingi na mwendo wa polepole.

Jongoo ni viumbe wadogo kutoka kundi kubwa la viumbe hai linalofahamika kama arthropoda. Kundi hili kubwa limejumuisha aina mbali mbali za wadudu warukao na watambaao.

Kundi hili nalo limegawanyika katika makundi mengine madogo ikiwemo Diplopoda ambalo linajumuisha aina mbalimbali za Jongoo.

Tofauti na aina nyingi za wadudu, mwili wa jongoo una pingili nyingi kuanzia 11 hadi 100 huku idadi hiyo ikitofautiana kati ya aina moja ya jongoo na nyingine.

Sifa kubwa ya Jongoo ni miguu mingi. Tabia hii imesababisha Jongoo kupewa Jina la “Millipede” kutoka kwenye lugha ya kilatini likimaanisha Miguu 1000.

Jongoo wana angalau jozi 200 za miguu, ambapo kila pingili ya mwili wake imebeba jozi mbili za miguu isipokuwa sehemu ya kwanza (ya kichwa) na sehemu tatu, ambazo kila moja ina jozi moja ya miguu.

Ingawa mwonekano wake huwatisha wengi, Jongoo ni kiumbe mtulivu sana ambaye muda wote hutembea polepole.

Mdudu huyu ana uoni hafifu hivyo maisha yake yanaongozwa kwa njia ya kuhisi kupitia antenna zake za kichwani. Antenna hizi zinamwezesha kujua uelekeao anaoenda, kutambua mazingira yake pamoja na kuhisi hatari inayomzunguka.

Anapohisi hatari hujiviringisha akificha sehemu zake muhimu kama kichwa huku akitoa majimaji yenye kemikali ya kuwachefua maadui ili wasimguse.
Jongoo ametambuliwa na wataalamu wa mazingira kama mtengeneza mazingira. Anatumia vitu vilivyokufa kama chakula na hivyo kuzalisha nishati na hivyo kufanya virutubisho kuendelea kuzunguka mazingira aliyopo jongoo.
Ni jukumu letu wote kuyatunza mazingira yetu ili viume hai hivi viendelee kuwepo na hivyo kudumisha na kuendeleza Bayonuwai , ili vizazi vijavyo navyo vifaidike.

Likes:
0 0
Views:
2163
Article Categories:
Wildlife