Mfahamu Nyani Kipunji kutoka Hifadhi ya Mlima Rungwe

Kipunji (Rungweceubus Kipunji) ni jamii mpya ya nyani waliogunduliwa mwaka 2003, ni aina ya tumbili wanaopatikana na kuishi katika misitu ya Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania.

Wanasayansi waliwaita jamii hii mpya Rungweceubus kutokana kwamba wanapatikana katika Mlima Rungwe na maeneo mengine yanayoizunguka milima hiyo tu.

Kipunji ambaye aligunduliwa na Shirika la Kimataifa la Hifadhi ya Mazingira na Viumbe Hai (WCS) mwaka 2003 katika msitu mlima Rungwe ambao uko juu 2,981km kutoka usawa wa bahari ni moja kati ya hifadhi za asili ambayo rasilimali pekee ya Taifa inayohitaji kutunzwa mazingira yake.

Nyani Kipunji ni mnyama mwenye aibu ambaye kumwona kwake kunahitaji tahadhari na inawezekana kwa siku mbili au tatu asionekane ingawa kuna wakati hutembea kwa makundi.

Kipunji anakula vyakula vya aina tofauti vikiwepo majani machanga na yaliyokomaa, maua, matunda mabichi na yaliyoiva na mazao ya shambani kama mahindi, viazi n.k.

Likes:
0 0
Views:
648
Article Categories:
Wildlife