Tembo wa Manyara

Tembo wa Manyara ni jamii ya tembo wenye asili ya Afrika wanaopatikana Kusini mwa Jangwa la Sahara

Tembo hawa wanaishi kwenye makundi ya rika tofauti tofauti ikijumuisha tembo wakubwa na watoto na katikati. Katika kundi la tembo kiongozi anakuwa jike mkubwa akiwa ndiye mwenye jukumu la kuhakikisha kundi liko salama wakati wote.

Maajabu ya mnyama huyu ni kuwa hutumia muda mrefu zaidi kula chakula takribani saa 20na muda unaobaki hutumia kupumzika. Chakula chake kwa siku hujumuisha takribani lita 200 za maji na kilo 150 za chakula.

Tembo hubeba mimba kwa miezi 22, mara nyingi huzaa mtoto mmoja, mara chache huzaa mapacha, na ukali wake huonekana kwa urahisi anapokuwa na mtoto wake.

Katika Hifadhi ya Ziwa Manyara ni moja ya maeneo machache utakayoweza kuona makundi makubwa ya Tembo ndani ya eneo dogo na kwa muda mfupi na kwa ukaribu zaidi.

Likes:
0 0
Views:
682
Article Tags:
Article Categories:
Wildlife