Viumbe vya ajabu vinavyotumika kwenye tiba

Bidhaa mbalimbali za wanyama na mimea zimekuwa zikitumika kama tiba kwa miaka mingi sasa huku dawa nyingine zikithibitishwa kutumika kama dawa asilia.

Vipo pia baadhi ya viumbe ambavyo vimekuwa vikitumika kutibu matatizo mbalimbali vinavyoweza kukuacha mdomo wazi akiwemo Funza.

Pale ambapo mgonjwa hupatiwa matibabu ambayo hayaoneshi matokeo mazuri wadudu hawa wa ajabu huletwa kufanya kazi ambayo madaktari na dawa za kisasa hawawezi wakati mwingine.

Funza ni walafi na hula nyama yenye magonjwa na inayokufa. Hivyo kuwafanya tiba nzuri kwa wale wenye madonda sugu.

“Funza watageuza jeraha la muda mrefu kuwa jipya papo hapo kwa siku chache kwa kula tishu sugu na bakteria. Kutoka hapo kidonda kinatibika na hatimaye kinaweza kupona,” anasema Dkt. Edgar Mayens Jr., daktari wa upasuaji wa ngozi Oregon.

Konokono

konokono aina ya ‘cone snail’ huyu anaishi baharini na hula samaki. hutumia sumu yake na kuua mawindo yaliyo karibu.

Aina mbalimbali za konokono hawa wana misombo kati ya 150-200 ambazo hutofautiana kati ya konokono.

Mnamo 2004, FDA iliidhinisha matumizi ya dawa ya maumivu ya ziconotide, iliyouzwa kama Prialt, inayotokana na moja ya protini za konopeptidi kutoka kwa sumu ya konokono. Matumizi mengine yanayoweza kutumika kwa misombo kutoka kwa sumu ya konokono ni pamoja na dawa za maumivu ya neva, kifafa, ugonjwa wa moyo na kiharusi.

Likes:
0 0
Views:
505
Article Tags:
Article Categories:
TourismWildlife