Waandishi wa Habari Afrika watembelea vivutio vya Utalii Arusha

Baada ya kuadhimisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani iliyofanyika Mei 3 jijini Arusha, waandishi wa habari na wadau wengine wa habari kutoka nchi mbalimbali za Afrika wametembelea vivutio vya utalii mkoani humo kujionea uzuri wa Tanzania.

Vivutio vya utalii walivyotembelea ni Hifadhi ya Taifa Terangire, Hifadhi ya Ngorongoro, Hifadhi ya Taifa Manyara na Hifadhi ya Taifa Arusha.

Uamuzi wa waandishi wa Habari kutembelea vivutio hivyo utavitangaza katika nchi mbalimbali za Afrika na  kuvutia watalii zaidi, hivyo kuendana na mkakati wa sasa wa serikali kutangaza utalii na fursa za utalii na uwekezaji kupitia filamu ya Tanzania: The Royal Tour.

Waandishi hao wamepongeza jitihada zinazofanywa na serikali kutangaza utalii pamoja na kuhakikisha vivutio hivyo vinalindwa ili kuweza kukirithisha kizazi kijacho. Kwa kauli moja wamesema kuwa ni jukumu lao kutangaza mazuri ya Afrika, ili uzuri wake wa mandhari na watu utambulike duniani badala ya  kutambulika kwa umaskini, njaa, migogoro na vita.

Likes:
0 0
Views:
29
Article Categories:
Wildlife