Wafahamu Mwari, ndege wanaoruka kutoka Asia na Ulaya hadi Tanzania

Mwari Mweupe ni ndege wakubwa aina ya bata maji wanaopatikana kwa wingi Ziwa Rukwa kwa nchi ya Tanzania.

Ni ndege wakubwa zaidi wanaoweza kutofautishwa kwa kuwa na miguu yenye vidole vyote 4 vya utando ambavyo hujulikana kama ‘totipalmate’

Ndege hawa hutokea bara la Ulaya na Asia na huja Afrika kwa ajili ya kutafuta chakula kwani ndio sababu ya msingi inayowafanya kuhama mara kwa mara kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Mwari hula samaki pamoja na wanyama wadogo wasio na uti wa mgongo. Ndege hawa wa majini hawalazimiki kupiga mbizi ili kukamata mawindo yao, badala yake hutumia mdomo wao mrefu kuingiza samaki midomoni mwao kwa kutumbukiza vichwa vyao majini.

Zoezi la kupata samaki hao majini wakati  mwingine hufanywa kwa ushirikiano, ambapo Mwari kadhaa husogea kwenye duara ili kuwachanganya samaki na kutumbukiza vichwa vyao ndani ya maji kwa pamoja ili kuwakamata samaki, njia hii ina mafanikio zaidi kwao.

Kwa kila Mwari huhitaji takribani kilogramu 0.5 hadi 1 ya samaki kila siku kwa ajili ya mlo wake.

Likes:
0 0
Views:
842
Article Categories:
Wildlife