Wahitimu watakiwa kuongeza tija sekta ya utalii

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Juma Mkomi amewataka Maafisa na Askari wa Uhifadhi waliohitimu mafunzo ya kijeshi kuhakikisha wanalinda vivutio vya utalii vilivyopo nchini na kuongeza kuwa Filamu ya ‘Tanzania: The Royal Tour’ iliyozinduliwa hivi karibuni na Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan haitakuwa na maana kama vivutio hivyo havitalindwa

Amesema hayo akifunga mafunzo ya kijeshi kwa Maafisa na Askari 190 kutoka TFS, TANAPA, NCAA na TAWA katika kambi ya mafunzo ya kijeshi Mlele mkoani Katavi, na kuwataka kutumia mafunzo hayo kuimarisha sekta ya utalii.

”Filamu ile imezinduliwa kwa lengo la kuhamasisha shughuli za utalii na Uwekezaji nchini na tangu izinduliwe kila Mtanzania na dunia inafahamu Tanzania kuna nini,” amesema.

Kwa upande wake Mratibu wa Jeshi la Uhifadhi, Fidelis Kapalata amesema mafunzo hayo waliyoyapata katika yanakwenda kubadili mfumo wao kufanya kazi hususan katika kipindi hiki ambacho ujio wa watalii utakuwa mkubwa kufuatia kuzinduliwa kwa Filamu maarufu ya Royal Tour

Katika mahafali hayo, Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Filberto Sanga ameiomba Wizara ya Maliasili na Utalii kuangalia uwezekano wa kuwapangia kazi wilayani mwake baadhi ya wahitimu kutoka kila taasisi ya uhifadhi ili waweze kulinda maliasili zilizopo mkoani Katavi kwa kile alichodai mkoa huo umebarikiwa vivutio vingi vya utalii na vingi vikiwa wilayani Mlele.

Likes:
0 0
Views:
37
Article Categories:
TourismWildlife