Kaburi la Baba yake Chifu Mkwawa

Baba yake Chifu Mkwawa alijulikana kwa jina la Munyigumba Tengamahumba Chengamahomelo Muhomiyao Muyinga ambaye anasadikiwa kufariki miaka ya 1860 na kuzikwa katika kaburi lililopo Iringa kijiji cha Rungemba Halmashauri ya Mafinga wilayani Mufindi.

Baba yake Mkwawa alizikwa na mtu hai aliyefahamika kwa jina la
Segeleni Mwang’owo aliyeingia kwenye kaburi na kumpakata marehemu na kuzikwa naye ambapo zamani ilikuwa ni fahari kuzikwa na Chifu hivyo watu wengi kugombea kuzikwa na Chifu.

Alipewa jina la Tengamahumba kwa sababu ya kuunganisha makabila kama vile Wahehe, Wazungwa, Wasagara na Wabena kuwa kitu kimoja.

Jina laChengamahomelo lilitokana na kutengeneza zana za kivita mwenyewe na jina la Muhomiyao kwa sababu wakati wa mapigano
alikuwa havuki kwenye himaya ya mtu mwingine alipigania kwenye himaya yake tu.

Pembeni ya kaburi lake kuna kaburi la mtoto wake yaani kaka yake na Mkwawa aliyefahamika kwa jina la Msengele Kilekamagana Munyigumba Mwamuyinga ambaye awali baada ya kufariki alizikwa katika uwanja unaojulikana kwasasa kama uwanja wa Samora ambapo hata kwa kipindi hicho watu walikuwa wakicheza mpira hivyo mzimu wake ukataka kuhamishwa ili asikanyagwekanyagwe na wachezaji ndipo mwaka 1974 wazee wakaitikia wito huo na wakaliamisha kaburi lake na kuliweka pembeni ya Baba yake.

Likes:
0 0
Views:
902
Article Categories:
History