Kanisa la kilutheri Lupembe lilijengwa na wajerumani mwaka 1903 na kufunguliwa rasmi mwaka 1911 mkoani Njombe.

Wakati wa ujenzi wa kanisa hili wazawa chini ya Chifu Lupembe Hongoli walitumika kama nguvu kazi ambapo walikuwa wanalazimishwa kusomba maji kwa kichwa kutoka mtoni ,kukusanya mawe,kufyatua matofali ,pamoja na kupasua mbao kutoka katika misitu ya iditima ambayo mpaka sasa inamilikiwa na wakala wa misitu Tanzania.

Baada ya vita vya kwanza kati ya waingereza na wajerumani jengo hili halikutumika tena kwa ajili ya ibada bali lilitumika, kwaajili ya kuhifadhia silaha za kivita.

Mpaka sasa kanisa hili linaendelea kuhifadhi historia yake ikiwa pamoja na mabaki ya silaha za zamani zilizokuwa zinatumiwa na Muingereza katika vita vya kwanza vya dunia.