Kilikuwa chuo cha wapigania uhuru

Imeandikwa na Happyness Hans

Baada ya Tanzania kupata uhuru mwaka 1961, Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ambaye aliwahi kuwa Mwenyekiti wa nchi zilizokuwa msitari wa mbele katika ukombozi wa Bara la Afrika, alitoa eneo hili kwa wapigania uhuru wa nchi jirani.

Kwa vile wakoloni wengine ilikiwa si rahisi kuwaondoa bila kutumia mtutu wa bunduki, wapigania uhuru walitakiwa kupata hapa mafunzo ya kijeshi ili kuyatumia katika harakati za kukomboa nchi zao kutoka kwenye makucha ya wakoloni. Baadhi ya nchi hizo ni Msumbiji na Zimbabwe.

Miongoni mwa viongozi waliopita hapa na kupikwa kijeshi ni Rais wa kwanza wa Msumbiji huru, Hayati Samora Machel, pamoja na Hayati Robert Mugabe wa Zimbabwe.

Hata Rais wa sasa wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa alipozuru Tanzania mwaka 2018 alitembelea chuo hiki na kutoa kiasi cha dola elfu kumi kwa mkuu wa chuo ili kusaidia mambo mbalimbali ikiwemo ukarabati.

Likes:
0 0
Views:
172
Article Categories:
History