Makumbusho ya Tanga yenye urithi muhimu

By Happyness Hans

Jengo hili ambalo lina kumbukumbu muhimu lilijengwa na Wajerumani mwaka 1890 chini ya Kiongozi wao, Paul Illare ambaye alikuwa analitumia kwa shughuli za utawala na pia alilitumia kama Ikulu yake pamoja na makazi.

Maeneo aliyotawala Mjerumani huyu ni Tanga, Kilimanjaro pamoja na Arusha,

Eneo hili lina vitu mbalimbali ambavyo vilijengwa na Wajerumani na mpaka leo vipo ikiwemo feni ya mwaka 1932, milango imara isiyoharibika na marumaru imara.

Wajerumani waliondoka rasmi kwenye makazi haya na kuchukuliwa na Waingereza baada ya kupigwa katika Vita vya Kwanza vya Dunia mwaka 1918.

Baada ya uhuru wa Tanganyika mwaka 1961 aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mangungi Mwilu aliweka kambi katika jengo hili pamoja na kuendesha shughuli za kiutawala. Serikali ililiachia jengo hili rasmi mwaka 2003.

Ili kuboresha ubora wa jengo, mwaka 2006 Taasisi ya Urithi iliiomba Serikali kuchukua jengo hili na kulikarabati ili liweze kutumika kama makumbusho ya Tanga. Serikali ilikubali na mwaka huo wa 2006 ukarabati ulianza na kumalizika rasmi 2007 na makumbusho ya Tanga ikazaliwa rasmi.

Usikose kufanya utalii wa ndani kwa kutembelea Makumbusho haya bila kusahau kufuatilia Safari Channel ili kujua urithi wetu, vivutio vya utalii na mengine lukuki.

Likes:
0 0
Views:
293
Article Categories:
HistoryTSC