Mnara wa saa Tanga

By: Happyness Hans

Mnara huu wa saa, ulitengenezwa mwaka 1901. Asili yake inahusishwa na Vita vya Abushiri vilivyorindima mwaka 1888 hadi 1889.

Inaelezwa kwamba Waajemi walikuja eneo hili la Pwani ya Afrika Mashariki kwa ajili ya biashara zao. Kutokana na utaratibu wa Wajerumani wa kutumia mizinga ya rangi kwa ajili ya kujihami walitoa ishara kwa Waajemi hao. Lakini walipotoa ishara hiyo ya mizinga ya rangi Waajemi walikaa kimya bila kutoa ishara yoyote ya kuonesha kuwa wao sio maadui, hali iliyopelekea Wajerumani kuwalipua wakidhani ni maadui zao kwa maana ya askari wa Abushiri.

Baadaye Wajerumani waligundua wamekosea kwa kuua watu wasiohusika, wakawazika na kuwajengea mnara huu na kuweka saa iwe kama kumbukumbu ya tukio hilo, wakiamini kuwa ni njia ya kuwaomba msamaha watu waliowaua bila ya makosa.

Njoo utembelee historia hii bila kusahau kufuatilia Safari channel kujionea na kujifunza mengi kuhusu vivutio lukuki vya Tanzania.

Likes:
0 0
Views:
83
Article Categories:
HistoryTSC