Imeandikwa na: Happyness Hans
Hii ni nyumba aliyokuwa anaishi mfanyabiashara mwenye asili ya Kiarabu, Said Ally Mohamedi na ndio eneo lililosababisha kupatikana kwa jina la Saadani. Hapo awali mahali hapa palikuwa panajulikana kwa jina la Utondwe.
Mfanyabiashara huyo, Said Ally Mohamedi alikuwa ana saa yake ya ukutani ambayo aliamua kuiweka kwenye duka lake.
Lakini kutokana na kuchoshwa na watu kumuuliza saa kila wakati, aliona vyema aihamishie saa yake ndani. Kutokana na hatua hiyo watu waliokuwa wakienda dukani hapo walianza kuuliza: “Saa iko wapi?”
Katika kuwajibu kwa Kiswahili chake cha ‘kubabia’, Said alikuwa akijibu: “Saadani” badala ya “saa iko ndani” na ndio ukawa mwanzo wa eneo hili kuitwa Saadani.