Utalii wa baharini kwa kutumia Boti ya Kioo

Hii ni boti ya kisasa ambayo imetengenezwa na Watanzania kwa ajili ya kufanya utalii wa baharini kama vile kuona samaki kupitia kioo cha chini ya boti hiyo kinachoonesha mandhari ya chini ya bahari.

Ukiwa ndani ya boti hii unaweza kuona viumbe hai waliopo chini ya bahari kama vile samaki, matumbawe pamoja na mwani ukiwa katika kina kifupi cha bahari.

Boti hiyo inayosimamiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA) ni moja ya vivutio vya utalii katika mji wa Kilwa kwani wageni wengi hupendelea kukodi na kufanya utalii wa kuvua samaki na kutembelea katika eneo la fukwe asili lililopo Songo Mnara, Kilwa mkoani Lindi.

Likes:
0 0
Views:
625
Article Tags:
Article Categories:
HistoryTourism