Wananchi kugawiwa miche miti ili kulinda mazingira

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja amewataka wananchi kuwa wazalendo kwa kuitunza miche ya miti watakayokabidhiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) ili iweze kuleta matokeo chanya ya kuhifadhi mazingira.

Amesema hayo akikagua mradi wa kitalu cha miche ya miti wenye thamani ya shilingi milioni 43 unaosimamiwa na TFS katika wilaya ya Magu mkoani Mwanza.

Amesema katika utekelezaji wa mradi huo, awamu ya kwanza zimetolewa fedha kiasi cha shilingi milioni 17 ambapo Serikali itaendelea kutoa fedha kwa awamu nyingine ili kukamilisha mradi.

Kaimu Kamanda wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Kanda ya Ziwa, Thomas Moshi amesema kitalu hicho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha miche laki tatu kwa mwaka, hivyo kuendelea kuihudumia jamii ili kuhakikisha maeneo ambayo hayana miti uoto wa asili unarudi.

Likes:
0 0
Views:
417
Article Tags:
Article Categories:
HistoryTourism