Mlima wa Hija Milanzi

Mlima Itwelele wenye maajabu yake unapatikana wilayani Sumbawanga kata ya Milanzi mkoani Rukwa.

Kama ilivyo tafsiri ya neno Hija kwa imani ya dini ya Kiislamu, Wakristo nao katika mkoa wa Rukwa hawajaachwa nyuma na utaratibu wa kuhiji.

Wenyeji wa Sumbawanga wanasema kuwa
ifikapo mwezi Septemba kila mwaka kuanzia tarehe 14 ama Jumapili ya pili ya mwezi huo, ibada maalumu ya Hija hufanyika katika mlima huo.

Parokia zote za mkoa wa Rukwa za kanisa Katoliki hufika hapo kuhiji.

Katika kumbukumbu inaonekana Msalaba uliopo kileleni mwa mlima huo ulisimikwa rasmi mwaka 2001.

Inaelezwa kuwa kwa imani ya kanisa Katoliki, kila mwaka kuna ibada inahusu kutukuka kwa msalaba, hivyo katika kalenda zao mkoani Rukwa wakaona ni vema ifanyike Hija mahali hapo ambapo maelfu hufunga safari kutoka maeneo mbalimbali na kufika hapo kwa maombi, sala na dua japo wengine huenda kwa ajili ya mapumziko au kutalii.

Kwa upande wa tamaduni za asili za wakazi wa Sumbawanga inaelezwa kuwa, watu wa kabila la wafipa kipindi cha miaka ya nyuma nao walikuwa na utaratibu wa kufanya ibada mara moja kwa mwaka wakiomba kwa mababu waliokwisha tangulia mbele ya haki kama sehemu ya ibada zao,

Likes:
0 0
Views:
765
Article Categories:
Southern Zone