Hifadhi ya Msitu Pindiro

Hifadhi ya Msitu wa Mazingira Asilia Pindiro (PNFR) ni Sehemu ya misitu ya Pwani ya Tanzania unaopatikana katika mkoa wa Lindi wilayani Kilwa.

Hifadhi hii ya msitu Pindiro ina eneo la hekta 12,249 na urefu wa mpaka wake ni kilomita 55.34 na inapatikana katika mwinuko wa mita 140 juu ya usawa wa bahari.

Misitu hii ya pwani ya Afrika Mashariki ikiwa ni pamoja na msitu wa hifadhi Pindiro inachukuliwa kuwa maeneo muhimu ya ulimwengu yaliyosheheni baianuai.

Ulitangazwa kuwa msitu wa hifadhi mwaka 1956 kutokana na umuhimu wake wa kuwa lindimaji ambapo una vyanzo viwili vya maji ambavyo ni Matawanga katika mteremko wa Kusini na Mashariki mwa kilima cha Mbarawala ambacho ndio chanzo cha maji ya umwagiliaji kwenye mashamba

Chanzo cha pili ni kwenye mteremko wa mlima uliopo mto nyange ambacho kinatengeneza bwawa la Nyange (bwawa la viboko) ambapo maji yake yanatiririka na kumwagwa mto Mbwemkulu.

Ukiwa ndani ya Hifadhi ya Msitu ya Pindiro unaweza kufanya utalii wa ekolojia, utalii wa kutembea kwa miguu na kushuhudia wanyama kama vile Tembo, Nyati, Nyani Pundamilia, swala na wanyama wakali kama vile Chui na Simba

Likes:
0 0
Views:
616
Article Categories:
Tourism