Historia ya Mapango ya Popo (Bat Caves)

Pango la popo linapatikana nje kidogo ya mji mdogo wa Songwe karibu na Mto Songwe (Songwe ya Kaskazini) wenye chanzo chake katika milima ya Umalila karibu na Santilya iliyopo kusini ya Mbeya ikielekea Kaskazini na kuishia Ziwa la Rukwa.

Pango hili ni makazi ya Popo ambayo ni moja ya vivutio vya kitalii na huvutia sana kuitembelea kwa kuwa imeumbwa kwa mwonekano wa aina yake na watofauti.

Pindi utembeleapo pango hilo unaweza kuingia kwa kupitia mlango wake mdogo kwa kulinganisha na mwonekano wake mkubwa uwapo ndani, ambapo unashauriwa kuingia na tochi yenye mwanga mkali ili kuweza kuepuka kutumbukia katika mashimo madogo madogo ndani ya mapango hayo na kuweza kulivuka kwa uangalifu daraja dogo linalounganisha pande mbili za pango iliyotengenezwa na binadamu ndani ya pango hilo.

Pia baada ya kuvuka daraja hilo unaweza kupata mwanga kupitia shimo/tundu ambalo hupenya mpaka nje kwa kupita mwonekano wa juu wa pango hilo.

Utembeleapo mapango hayo utapata hali ya hewa nzuri ya joto kwani mkoa wa Songwe una hali ya hewa ya baridi, uoto wa asili uliotawaliwa na miombo, kuwaona wanyama wadogo wadogo kama sungura pori (Hare), mwonekano mzuri wa safu za milima na Mto Songwe, viwanda vya utengenezaji wa vifaa vya ujenzi kama chokaa, simenti na marumaru, kuujua mji wa songwe na visima vya asili ya maji moto.

Likes:
0 0
Views:
620
Article Categories:
Tourism