Idadi ya Watalii nchini yaongezeka kwa asilimia 63

Jumla ya Watalii 742,133 wameingia nchini katika kipindi cha Januari hadi Julai 2022, ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 62.7, ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 2021, ambacho kilishuhudia ujio wa watalii 456,266.

Kwa mujibu wa takwibu za Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS),kati ya watalii hao wa mwaka 2022, Watalii 222,449 sawa na asilimia 30 waliingia nchini wakitokea Zanzibar.

Katika kipindi tajwa, Marekani iliongoza kuingiza Watalii wengi zaidi nchini kwa nchi zilizo nje ya Afrika ikifuatiwa na Ufaransa, Ujerumani, Poland, Uingereza.

Kwa nchi za Afrika, Kenya imeongoza ikifuatiwa na Burundi, Malawi, Uganda na Afrika Kusini.

Ili kufikia lengo la Watalii milioni 5 kwa mwaka ifikapo mwaka 2025, wadau katika sekta ya utalii wamehimizwa kuboresha huduma zao kuhakikisha wageni wanaokuja nchini wanakuwa mabalozi wa kuitangaza Tanzania.

Likes:
0 0
Views:
539
Article Tags:
Article Categories:
Tourism