Kampuni ya Hong Kong kutangaza vivutio vya Tanzania

Kampuni ya REO Communications kutoka Hong Kong inayojishughulisha na utangazaji wa maeneo ya uwekezaji ya nchi mbalimbali barani Afrika kwa njia ya majarida imeonesha utayari wa kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini.

Hayo yamefahamika katika kikao kati ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja na watendaji wa kampuni jijini Dodoma ambapo amewapongeza kwa nia nzuri ya kutaka kutangaza maeneo ya uwekezaji pamoja na vivutio vya utalii vya Tanzania.

Ameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha katika kuhakikisha wanafanikiwa katika adhima hiyo.

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya REO Communications nchini Tanzania, Xhovana Kelmendi amesema lengo ni kuhakikisha wanatangaza maeneo ya uwekezaji katika sekta mbalimbali ikiwamo Utalii, Kilimo, Madini n.k.

Amesema wameshafanikiwa kutangaza maeneo ya uwekezaji katika nchi ya Indonesia na wana miradi ya aina hiyo ambayo inaendelea katika nchi za Kuwait, Morocco, Nigeria, Malta na Tokyo.

Kikao hicho ni mwendelezo wa vikao vya kukutana na wadau wa Sekta ya Maliasili na Utalii kwa lengo la kuhakikisha idadi ya watalii inaongezeka.

Likes:
0 0
Views:
389
Article Tags:
Article Categories:
Tourism