Kifahamu Kimondo cha Sanza

Unapotaja kimondo kizito hapa nchini hutaacha kukitaja Kimondo cha Sanza kilichoanguka kutoka angani mwaka 1973.

Mnamo 1987 kimondo hiki kilisogezwa karibu na Kanisa Katoliki la Sanza linaloongozwa na wamisonari wa Consolata wilayani Manyoni mkoani Singida.

Kimondo, hiki ni kinatajwa kuwa miongoni mwa vimondo vizito kuwahi kutokea nchini Tanzania licha ya kutojulikana sana kwa Watanzania walio wengi baada ya kimondo cha Mbozi mkoani Songwe kinachoelezwa kuwa na urefu wa zaidi ya Mita 3.

Uongozi wa Kanisa Katoliki la Sanza linakusudia kujenga banda maalum la kutunzia kimondo hiki kama sehemu ya makumbusho ya kuhifadhi mambo mbalimbali ya kihistoria ili kuvutia watalii kutoka ndani na nje ya nchi lakini pia kama sehemu ya wanafunzi wa shule kujifunza kwa vitendo.

Tanzaniasafarichannel#utalii#kimondo#meteor#sanza#manyoni#singida