Kijiji cha Nyuki na utajiri wa vivutio vya utalii

Uzalishaji wa asali katika kijiji cha nyuki kilichopo katika kata ya Kisaji mkoani Singida ni miongoni mwa vivutio vikubwa vya utalii vinavyopatikana kijijini hapo.

Asali katika kijiji cha nyuki inaelezwa kuwa na matumizi mengi ikiwemo chakula, kiburudisho kwenye chai, dawa lakini pia malighafi muhimu viwandani.

Sumu ya Nyuki nayo imetajwa kuwa miongoni mwa malighafi muhimu inayozalishwa hapa na kuuzwa kwa gharama kubwa ndani na nje ya nchi ambapo kilo moja ya sumu hiyo inauzwa kwa shilingi milioni 100

Maporomoko ya maji yalipo ndani ya kijiji cha nyuki kutokana na uhifadhi wa mazingira ni eneo jingine muhimu linalochochea shuguli za utalii ndani ya kijiji.

Hayo ni baadhi ya mambo machache tuliyokujuza kutoka kijiji cha Nyuki mkoani Singida Je,nini kimekuvutia kwenye kijiji cha nyuki.

tanzania #tanzaniasafarichanel #ifoneo #kijijichanyuki #singida

Likes:
0 0
Views:
708
Article Categories:
Tourism