Kisa cha Siafu na msemo wa ‘Umoja ni Nguvu’

Siafu, mdudu mdogo jamii ya sisimizi isipokuwa yeye ana rangi nyekundu na kichwa imara kuliko sisimizi. 

Siafu wanaishi katika makundi kubwa huku mara nyingi wakionekana katika misafara kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Takwimu zinaonesha kuwa kundi moja linaweza undwa na hadi Siafu milioni 20 au zaidi. 

Wadudu hawa wadogo wamekuwa darasa na kielelezo cha kuuthibitisha ule msemo wa “umoja ni nguvu.”

Mshikamano wa Siafu katika kundi bado ni kitendawili kwa watafiti kwani baadhi wamedai kuwa ni harufu na wengine bado wanaendeleza tafiti hii.

Swali la kujiuliza, ikiwa Siafu wanaishi katika kundi kubwa, Je! Mgawanyo wao wa majukumu ukoje? Je! Wote wanatamia mayai? Je! Wote wanaenda kutafuta chakula? 

Kundi la Siafu linaundwa na Malkia, Mfalme, Wafanyakazi na Walinzi. Ambapo, kazi ya Malkia ni kutaga mayai huku Mfalme akiwa baba. Wafanyakazi hutafuta chakula cha malkia na kuhudumia mayai yake.

Je! Umewahi kukanyaga msafara wa Siafu? 

Hata uwe mbabe kiasi gani huwezi kujizuia kujikung’uta ili kuondokana na shambiulio la wadudu hawa wenye makali. Watafiti wanaeleza kuwa mashambulizi hayo hufanywa na Siafu walinzi.

Chakula kinapopungua katika eneo wanaloishi, inasababisha Siafu wachukue maamuzi ya kuhama na kutafuta sehemu nyingine yenye chakula cha kutosha. Wakiwa katika harakati za kuhama, wanatengeneza msafara na msafara wao unaweza kuwa na urefu wa kilomita elfu moja au zaidi.

Huku pembeni wanakuwa walinzi na mbele ya msafara pia wanatangulia walinzi wakiwa na mamlaka yakuhakikisha usalama katika kundi. Na wanapokutana na chochote njiani, Sifau walinzi wanakabiliana nacho aidha awe ni Binaadamu au mnyama. Na ikiwa ni mnyama mdogo mathalani Panya, wanaweza mng’ata na kumsabababishia majeraha makubwa sana au hata kufa.

Hii imetajwa kusababishwa na umahiri, ujasiri na ushujaa wa meno ya Siafu. Meno yake yanatajwa kung’ang’ania ngozi au sehemu yoyote atakayo ng’ata kiasi ambacho unaweza hata kutoa kiwiliwili lakini kichwa kikabaki paleplae.

Licha ya kuwa na uwezo mkubwa wa kung’ata bado Siafu hana masikio, hivyo anasikia kwa kutumia vinasa mitetemeko ya ardhi vilivyopo katika miguu yao. 

Uwezo wake mkubwa wa kubeba vitu vizito mara kumi hadi hamsini ya uzito wake unamfanya Siafu kutambulika kama moja ya wadudu mahiri na shupavu. Kwani ukilinganisha na binadamu, watafiti wamefananisha uwezo huo wa Siafu kuwa ni sawa na binadamu mwenye kilogramu 90 hadi 100 anyanyue na kubeba gari dogo kichwani.

Hii ni Tanzania, yote haya utayapata hapa

Tanzania safari channel

Likes:
0 0
Views:
1315
Article Categories:
Tourism