Lifahamu Pori la akiba Rungwa

Pori la akiba Rungwa lenye ukubwa wa kilometa za mraba 9000 lililopo Itigi wilayani Manyoni, ni miongoni mwa vivutio vya utalii vinavyopatikana ndani ya mkoa wa Singida. Pori hili ni la pili kwa ukubwa kati ya mapori 22 nchini Tanzania baada ya pori la akiba la Selous ambapo jumla ya mapori yote yanaelezwa kuwa na kilometa za mraba zaidi ya elfu 70.

Utalii wa uwindaji wa wanyama mbalimbali katika pori la Rungwa ni miongoni mwa shuguli za uatalii zinazofanyika husani kipindi cha kiangazi. Wanyama kama vile Simba, Nyati, Chui, Faru na Tembo ni miongoni mwa wanyama wanaopatikana kwenye pori hili.

Uwepo wa Bwawa Rungwa ndani ya pori hiyo unaotiririsha maji yake katika mto Ruaha ni sehemu ya uatalii ndani ya pori la Rungwa kutokana na uwepo wa mamba na viboko ndani ya bwawa hili.

@emmanuel9397 📷 @oliver_trx drone master🎥 @elia__stephano 🎥 #tanzaniasafarichannel#Utalii#Itigi #Rungwa#manyoni#singida