Maporomoko ya Kalambo, Rukwa

Maporomoko ya maji Kalambo ni maporomoko pekee yanayogawa mpaka wa nchi mbili Tanzania na Zambia.

Maporomoko hayo yapo katika kKijiji cha Kapozwa Kata ya Kisumba, Wilaya ya Kalambo, mkoa wa Rukwa.

Kivutio hicho cha utalii kimekuwa kikionekana na kutangazwa kuwa kipo nchi jirani, na hivyo kuiondoa Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zenye maporomoko yanayotambulika duniani.

Usahihi ni kuwa maporomoko hayo yapo katika kijiji cha Kapozwa ambacho pia kilianzishwa kutokana na imani kuwa ukienda kuoga katika maporomoko hayo utapooza.

Kwa kuambiwa hivyo, wananchi wenyeji wa eneo hilo walipaita kijiji jina la Kapozwa.

Likes:
0 0
Views:
786
Article Tags:
Article Categories:
Tourism