Pindiro na Utalii wakutumia mahema

Eneo hili ni zuri na salama kwa utalii wa kutembea kwa miguu na kulala kwenye mahema huku usiku ukiwa na utulivu na hali ya hewa nzuri inayotokana na wingi wa miti katika Msitu wa Hifadhi Pindiro.

Watalii wa ndani na nje ya nchi wengi wanapofika kutembelea Pindiro hupenda kulala kwenye mahema na kufurahia mandhari ya eneo hili lililopambwa na uoto wa asili huku pembeni kukiwa na vitanda vya kubembea.

Likes:
0 0
Views:
365
Article Categories:
Tourism