Reli kunufaisha utalii Saadani

Shirika la Reli Tanzania (TRC) lipo mbioni kukamilisha ukarabati wa kituo cha stesheni cha Mvave karibu na Hifadhi ya Taifa ya Saadani hivyo kuanza kutumiwa watalii watakaotembelea hifadhi hiyo.

Reli hiyo ya kisasa ya SGR itarahisisha usafiri kwa watalii kutoka Dar es Salaam hadi Saadani, Pwani badala ya kukodi magari.

TRC kwa kushirikiana na Mamlaka ya Hifadhi za Tanzania (TANAPA) wameweka juhudi kuhakikisha kuna miundombinu wezeshi kwenye maeneo ya utalii yanayofikika kwa usafiri wa treni.

Kamishina Msaidizi wa Uhifadhi Hifadhi ya Taifa Saadani, Ephraim Mbomo amesema hifadhi ina uwezo wa kuhudumia watalii takribani 300 kwa pamoja.

Ndani ya Saadani unaweza kujionea vivutio mbalimbali ikiwemo Faru, Simba, Chui, Nyati, Mbogo, Viboko, Swala, Ngiri, Mamba na wengine wengi ikiwemo mlango bahari unaounganisha Bahari ya Hindi.

Likes:
0 0
Views:
46
Article Tags:
Article Categories:
Tourism