Historia ya Nyumba ya Tembe mkoani Tabora

Miongoni mwa eneo lenye historia mkoani Tabora ni nyumba ya Tembe iliyopo Kwihara. Kituo hicho asili yake ni Biashara ya Utumwa, watumwa waliokuwa wakikusanywa kutoka mikoa ya Kigoma na nchi jirani walikuwa wakifikia hapo.

Eneo hilo asili yake hasa ni waarabu na sababu ya kukaa kwa wingi eneo hilo ni kutokana na Mtemi Swetu ambaye alikuwa anatawala miaka 1800 akiwa na mtoto wake Fundikira ambao walikuwa wafanyabiashara hivyo walikaribisha wafanyabiashara kutoka sehemu mbalimbali, kutokana na ukaribu huo waarabu wengi walijenga maeneo ya Kwihara.

Mwarabu ambaye alifanikiwa kuacha historia ni Said Salum Mohammed ambaye alijenga nyumba ya tembe mwaka 1857, kazi yake kubwa ilikuwa ni kukusanya watumwa kutoka kwa wafanyabiashara wadogo wadogo na kuwasafirisha kwa siku 45 hadi Bagamoyo kisha kupelekwa Zanzibar ambako kulikuwa na soko kuu la Watumwa.

Wakati waarabu wakiendelea kufanya biashara ya utumwa kulikuwepo na wageni wengine kutoka Ulaya na mmojawapo aliyefika eneo hilo ni mmisionari na mpelelezi Dkt. David Livingstone aliyefika mwaka 1871 na akakaribishwa kulala kwenye nyumba ya Said.

Ingawa alikaribishwa kwenye nyumba lakini Dkt. Livingstone hakukubaliana na biashara ambayo alikuwa akiiendesha mwenyeji wake na kupambana nae hadi akaamua kuondoka na kuelekea Sumbawanga kuendelea na biashara yake ya kununua watumwa.

Baada ya Said kuondoka, haikuchukua muda Dkt. Livingstone naye aliondoka na kuelekea Kigoma kwenda kulichunguza Ziwa Tanganyika, alipofika huko alikata mawasiliano na serikali yake ya Uingereza. Hali hiyo ilizua hofu huko Ulaya kwamba huenda Livingstone alikuwa ameshafariki.

Wazungu waliamini kuwa Dkt. Livingstone amefariki lakini Mhariri wa gazeti la New York Herald, James Gordon Bannett (Jnr) hakuamini habari hizo za kifo cha Dkt. Livingstone na aliamua kumtuma ripota wake mahiri Henry Morton Stanley kuja kumtafuta Dkt. Livingstone huku Afrika.

Stanley alikuwa ameajiriwa huko Marekani katika gazeti la New York Herald ingawa utaifa wake ulikuwa ni wa Uingereza, alifika Tabora mwaka 1871 akiongozana na rafiki yake aliyejulikana kwa jina Geroge William Shaw.

Baada ya kufika Tabora aliugua malaria na kumuacha Henry aelekee Kigoma kumtafuta Dkt. Livingstone ila baadaye Henry alikata tamaa ya kupona na kuamua kujipiga na kuzikwa eneo hilo ambapo mpaka sasa kaburi lake lipo.

Kwa ujumla jumba hilo limebeba historia ndefu ya mkoa wa Tabora kuanzia Waarabu hadi Waingereza.

Kwa simulizi ya kina kuhusu nyumba hii endelea kutazama Tanzania Safari Channel.

Likes:
0 0
Views:
976
Article Tags:
Article Categories:
Tourism