By Happyness Hans
Katika maeneo mengi ya Pwani likiwemo Jiji la Tanga, mara nyingi ni utaratibu wa kawaida kutumia “kawa” katika kufunikia chakula ili kisisogelewe na wadudu kama nzi, mende na hata vumbi.
Kawa hutengenezwa kwa kutumia ukiri na kunakshiwa na michoro mbalimbali pamoja na maneno ya kuvutia yenye kuchochea upendo hasusani kwa wanandoa. Upo hapo?
Mbali na urembo huo kwenye kawa kuna urembo mwingine kwenye vipepeo (vya kujipepea joto hasa kwa kuzingatia Tanga ni mji wa joto) ambavyo pia hupambwa kwa urembo na maandishi yenye kutoa ujumbe au kuvutia hisia mbalimbali.
Fuatilia haya ya utalii wa kitamaduni katika Safari Channel na pia tembelea Tanga kujua mengi kuhusu utamaduni wa watu wa Pwani.