Ilikuwa vita kati Fisi na Chui baada ya Chui kuporwa kitoweo chake.
Mara nyingi fisi huwaogopa wanyama kama vile Chui na Simba lakini wanapofanya mawindo yao fisi akiwepo karibu hupenda kupokonya na kuanza kula yeye.
Fisi hutambulika kwa jina la utani kama Bwana Afya maana yeye hupendelea kula mizoga ambayo wanyama wengine waliwinda, kazi inayochukuliwa ni kama kusafishisha mbuga.
Katika Hifadhi ya Taifa Serengeti upande wa Kaskazini tunashuhudia fisi akila mnyama ambaye amempora chui, na chui huyo amekaa pembeni na kumpisha fisi ashibe ndio na yeye aweze kula.