Watanzania kutazama filamu ya Royal Tour Mei 8

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Filamu ya Tanzania: The Royal Tour, Dkt. Hassan Abbasi amesema filamu hiyo itaoneshwa kwa wananchi wote kupitia vituo vya televisheni vya ndani Jumapili, Mei 8, 2022.

Mei nane ndio siku ya uzinduzi wa mwishi wa filamu hiyo nchini, utaofanyika Dar es Salaam sambamba na kurushwa kwenye televisheni ikiwemo Tanzania Safari Channel na TBC1, ameeleza Dkt. Abbasi ambaye pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Aidha, ameongeza kuwa wizara inafahamu shauku kubwa ya wananchi kuona kazi iliyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan kutangaza uwekezaji na utalii nchini.

Ili kuhakikisha wananchi wote wanaitizama na kuielewa filamu hiyo iliyorekodiwa kwa lugha ya Kiingereza changamoto za kuweka nukuu za KiSwahili zinaendelea.

Filamu hiyo inatarajiwa kuvutia watalii wengi zaidi, kuleta wawekezaji ambayo vyote kwa pamoja vitakuza pato la Taifa, ajira na kwanza na kuendelea kuitangaza Tanzania.

Likes:
0 0
Views:
446
Article Categories:
Tourism