Hifadhi ya Msitu wa West Kilimanjaro

Msitu wa hifadhi wa West Kilimanjaro una ukubwa wa hekari za mraba 7,532.01 uliopo upande wa magharibi wa Mlima Kilimanjaro, Wilaya ya Siha Mkoani Kilimanjaro.

Msitu huu unasimamiwa na Wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS).

Msitu wa West Kilimanjaro ni moja kati ya misitu 24 ya mashamba yenye sehemu ya misitu ya asili inayobeba vipengele mbalimbali vya utalii wa ikolojia. Ni eneo maarufu la bioanuwai ambalo lina mimea na wanyama kwa wingi.

Msitu huu pia ni kitovu cha utalii wa mazingira asilia na hivyo, kuwa kivutio kwa wawekezaji katika sekta ya utalii na shughuli za burudani.

Ndani ya msitu huo kuna njia za Ndege, Tembo, Mapango na mnara wa kutazama hifadhi ya mlima Donyomurwak, maeneo ya kuabudu na maeneo ya picnic.

Likes:
1 0
Views:
651
Article Categories:
Tourism