Waziri Chana: Bidhaa zote za misitu zipigwe chapa ya Tanzania

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Pindi Chana amewataka watengenezaji wote wa bidhaa za misitu nchini wahakikishe wanaweka alama inayoonesha bidhaa zao zimetengenezwa Tanzania “Made in Tanzania” ili bidhaa hizo zijulikane kuwa zimetengenezwa nchini.

Dkt. Balozi Pindi Chana ametoa kauli hiyo wilayani Mufindi wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea kiwanda cha DAZHONG HOOD kinachozalisha bidhaa zinazotokana na misitu na kubaini kuwa bidhaa zinazozalishwa na kiwanda hicho hazina alama inayoonesha kuwa zimetengenezwa Tanzania.

Waziri Chana amemtaka mmiliki wa kiwanda hicho Wu Bing ambaye ni raia wa China atekeleze agizo hilo na azingatie Sheria kanuni na taratibu za Tanzania.

Mbali na agizo hilo Waziri Dkt. Pindi Chana amepongeza juhudi za uhifadhi wa misitu nchini zinazofanywa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) .

Kwa upande wake Mbunge wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi amesema sekta ya Misitu ina mchango mkubwa kwa wananchi hasa wa Mafinga kwa kutoa ajira nyingi na mchango mkubwa kwenye Mapato ya Halimashauri hiyo kwa asilimia 60, hivyo yeye kama mwakilishi wa wananchi ataendelea kushirikiana na Wizara katika uhifadhi wa Maliasili hiyo.

Likes:
0 0
Views:
516
Article Categories:
Tourism