Team ya Safari Channel kuangazia REGROW Mbeya na Iringa

Timu ya wanahabari wa Tanzania Safari Channel na wanahabari kutoka vyombo vingine, imewasili Madibira mkoani Mbeya kuangazia mradi wa REGROW.

Timu hiyo ilipowasili imepokelewa na Naibu Msimamizi wa Mradi huo, Blanka Tengia, kisha wakafanya kikao ili kupata uelewa wa pamoja juu ya mradi huo, hususan katika eneo la Madibira na vijiji vya pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa Ruaha Mkoani Iringa.

Mradi huu unatekelezwa na Wizara ya Maliasili na Utalii na unalenga kuboresha usimamizi wa maliasili na kukuza utalii kusini mwa Tanzania.

Likes:
0 0
Views:
64
Article Categories:
TSC