Bandari kongwe ya Saadani

Imeandikwa na Happyness Hans

Bandari hii ya Saadani ni moja ya bandari kongwe nchini ambayo ilikuwa inatumika kusafirishia watumwa kwenda soko kuu la watumwa Zanzibar. Ilianza kutumika rasmi kwa shughuli hiyo tangu karne ya 19.

Historia inaonesha kwamba wavuvi kutoka maeneo mbalimbali katika karne ya 14 walijumuika na kuweka kambi katika eneo hili hata kabla haijaanza kutumiwa rasmi na wakoloni.

Kimsingi, eneo hili awali lilijulikana kwa jina la Utondwe lakini baada ya mfanyabiashara Said Ally Mohamedi kuwa anakosea kutamka neo “Saa iko ndani” kwa watu waliokuwa wanataka kujua muda na badala yake akawa ‘anachapia’ kwa kusema “saa dani”, watu wakaanza kusema “Tunakwenda pale kwa Saa Dani”, ndipo jina ilo likakamata na kuwa Saadani hadi leo huku jina la awali la Utondwe likitoweka. Vijana wa sasa hawalijui kabisa.

Haya pamoja na mengine lukuki ni mambo yanayokujia katika channel yako pendwa na pekee kwa masuala ya utalii nchini ya Safari Channel.

Likes:
0 0
Views:
94
Article Categories:
HistoryTourismUncategorized