Bidhaa ya kitalii ya vyungu

Vyungu ni bidhaa zinazotengenezwa kwa kutumia udongo wa mfinyanzi kwa matumizi ya kupikia, mapambo, kuwekea mapambo, kuweka joto kwenye vifaranga vya kuku, kuwekea mishumaa na kuhifadhia maji ya kunywa nk.

Bidhaa hizo zipo pembezoni mwa barabara kuu ya Iringa – Mbeya katika Kijiji cha Rungemba wilayani Mufindi katika Halmashauri ya Mji Mafinga ambapo watalii mbalimbali wakipita pembezoni mwa barabara hiyo huvutiwa navyo na hupenda kutembelea eneo hilo kwa kuangalia na kununua bidhaa hizo hivyo kuongeza pato kwa wananchi.

Vyungu hivyo vimenakshiwa kwa rangi na urembo tofauti tofauti jambo linalopelekea watu kuvutiwa kusimama mahali hapo.

Likes:
0 0
Views:
88
Article Categories:
Uncategorized