Hili ni kaburi la Chifu Rugaba Kasusura ambaye alikuwa Chifu wa nne wa kabila la Wasubi.Chifu Rugaba Kasusurandiye mkuu wa wilaya wa kwanza wa wilaya ya Biharamulo iliyopo mkoani Kagera baada ya Uhuru, na baada ya hapo akawa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Pia aliwahi kuwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.