Usilojua kuhusu kinyonga

Kinyonga ni aina za mijusi wenye ulimi mrefu unaonata na wenye uwezo wa kugeuka rangi ili kusaidia kurekebisha joto lao la mwili kutokana na kutokuwa na uwezo wa kuzalisha joto lao wenyewe.

Kinyonga anabadilika rangi kutokana na kuwa na seli zinazoangaza kwenye ngozi zao zikiwa na uwezo wa kusharabu mwanga/ joto ama kwa kukereka (mood) ili kujilinda. Kama ana hasira na hofu hugeuka rangi zisizong’aa kama rangi ya kahawia na akiwa na furaha hugeuka kwenye rangi zinazong’aa na kuonekana kwa urahisi kama vile kijani.

Jicho la Kinyonga lina uwezo wa kuona taswira mbili kwa wakati mmoja (360 degree) hiki ni kiwango cha juu sana miongoni mwa reptilia na wana uwezo wa kuona wadudu wadogo sana umbali wa mita 5-10.

Vinyonga wengine huwa na sumu kwa mfano kinyonga wa Namakwa ana sumu kiasi cha kuweza kumpofusha binadamu.

Miguu ya Kinyonga imeumbwa kwa namna ambayo inaweza kuparamia mazingira yoyote yale ya miti au miamba yaani iwe ya utelezi au hata miiba. Miguu yake inaweza kukunjika ama kukunjuka kama karatasi kulingana na mazingira.

Kwasasa ni nadra sana kuwaona vinyonga ndiyo maana analindwa na sheria za kimataifa za uhifadhi wa viumbe walio hatarini kutoweka.

Kinyonga huyu ameonekana Kalenga Iringa nje ya jumba la ukumbusho lililohifadhiwa fuvu la chifu Mkwawa.

Likes:
0 0
Views:
1806
Article Categories:
Uncategorized