Pindiro na uoto wa asili

Hifadhi ya msitu wa mazingira asilia Pindiro umepambwa na uoto wa asili wa Miombo na aina ya misitu ya pwani inayojumuisha zaidi ya aina 258 za miti ikiwemo minepa, mkongo, mninga, myombo, mrondondo, mpingo, mkunguti, msweli, mpugupugu, msenefu, mwaya na miti mingine

Eneo la Msitu wa hifadhi Pindiro limetawaliwa na misitu ya kijani kibichi katika ukingo wa Kusini na Mashariki mwa vilima vya Mbarawala haswa katika bonde la Nyange, misitu ya miombo na misitu ya wazi ( woodlands)

Watafiti na wanafunzi wengi huitumia Hifadhi ya Msitu Pindiro ili kupata taarifa sahihi za miti na dawa zitokanazo na miti hiyo na kufurahia hali ya hewa nzuri chini ya miti hiyo

Likes:
0 0
Views:
686
Article Tags:
Article Categories:
TourismWildlife