Rais Samia na Tanzania the Royal Tour, Los Angeles

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akitembelea kuangalia kazi za utayarishaji wa filamu mbalimbali katika Studio za Paramount Pictures Jijini Los Angeles nchini Marekani kabla ya uzinduzi wa Filamu ya Tanzania Royal Tour uzinduzi uliofanyika alfajiri ya leo katika Ukumbi wa Studio za Paramount.


Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Wabunifu mbalimbali pamoja na Wadau wakubwa wa Tasnia ya Filamu katika Jiji la Los Angeles ambapo alfajiri ya leo kumefanyika uzinduzi wa mara ya pili wa Filamu inayotangaza utalii wa Tanzania ‘Tanzania Royal Tour’.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Ronald Fenty Baba wa Msanii Maarufu Robyn Rihanna Fenty ambaye alifika katika ukumbi wa Paramount Pictures kwa ajili ya kuangalia Filamu ya Tanzania Royal Tour iliyozinduliwa alfajiri ya leo Los Angeles, Marekani.
Likes:
0 0
Views:
1420
Article Categories:
CaltureWildlife