Simba wanaopanda juu ya miti katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara.

Simba wanaopanda miti ni miongoni mwa vivutio vya wanyamapori vinavyoweza kuonekana kwenye Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara ambayo iko kaskazini mwa Tanzania.

Tabia ya kupanda miti miongoni mwa simba inaweza kuonekana katika maeneo yanayozunguka Afrika Mashariki kama vile Hifadhi ya Ziwa Manyara nchini Tanzania na pia katika Hifadhi ya Malkia Elizabeth nchini Uganda.

Tabia ya simba wanaopanda juu ya miti katika hifadhi ya ziwa Manyara imeelezwa kuwa ni njia mojawapo ya kujikinga na wadudu wanaookuwa chini.

Sababu nyingine ni kwamba wanafurahia upepo wa baridi kutoka juu ya mti na pia kupata mazingira mazuri ya kupumzika.

Kutoka juu kwenye miti, simba wanaweza pia kutazama mawindo yao katika tambarare za savanna.

Likes:
0 0
Views:
796
Article Tags:
Article Categories:
TourismWildlife